Burudani

Chanzo: Paul na Jude hawana shukrani, Lola aliwasaidia fedha kipindi hajafanikiwa

Shukrani ya punda ni mateke. Vyanzo mbalimbali vimedai kuwa familia ya P-Square ambayo inamchukulia mke wa Peter, Lola kama mwanamke mpenda fedha anayeutumia utajiri wa mume wake, imesahau jinsi mwanamke huyo alivyoanza uhusiano na Peter kipindi hakuna aliyekuwa akiwafahamu P-Squaree na walikuwa maskini wa kutupa.

peter okoye n wife
Peter na mkewe Lola

Wale wanaomfahamu Lola, wamesema kuwa pamoja na kuwa na umri mkubwa kumzidi Peter, hayupo naye kwasababu ya fedha zake bali kwakuwa ni kweli anampenda kwa dhati. Chanzo kimoja kimeiambia safu ya Razzmatazz ya gazeti la ‘Nigerian Tribune’ kuwa: P-Square haikuwa na chochote kipindi Peter ameanzisha uhusiano na Lola, na ni Lola ndiye aliyekuwa akiwasaidia fedha kipindi hicho na Jude, Paul na mama yao walikuwa wanafahamu. Walimtumia Lola kwakuwa alikuwa na connections zake lakini walipoanza kupata fedha ndipo walipojua kuwa ni mwanamke wa Kiyoruba ambaye haukuwa anafaa kuolewa na Peter.”

“Peter alimpenda Lola na kwasababu alisimama upande wake na kutomsikiliza mama yake na ndugu wengine, walianza kumghasi na kuyafanya maisha yake kuwa magumu. Mbaya zaidi alikuwa kaka yake Jude ambaye siku zote hajawahi kukumbali wala kumheshimu Lola.
Anaamini kuwa Lola alikuwa akijionesha tu wakati alipokuwa akiisaidia familia yao enzi hizo. Walikuwa wakichukua vyote alivyowapa lakini sasa hawamtaki na Peter hawezi kuruhusu hilo. Wanataka kumlipa kwa ubaya msichana wa watu na Mungu hawezi kuruhusu hilo,” alisema mtangazaji mmoja wa kike.

Aliendelea kusimulia:

Nakumbuka kipindi Peter alipokuwa akidate na Lola. Peter alikuwa alikuwa anaona aibu kumpeleka Lola nyumbani kwao, Ilupeju kipindi hicho. Ilikuwa ni nyumba ya vyumba viwili ambako watu sita walikuwa wakiishi wakiwemo dada zao ambao kwa sasa hawamtaki. Lola hakupenda kumng’ang’aniza Peter kwakuwa hakuwa anapenda. Lakini siku mpja Peter alikuwa mgonjwa. Lola alisikia kuhusu kuumwa kwa mpenzi wake na akamuomba rafiki yake aliyekuwa akipafahamu kwao kumpeleka. Ulikuwa ni ujio wa kushtukiza na wengi hawakuupenda. Aliwanunua air conditioners muda mfupi baada ya kuondoka. Alifanya yote hayo kwakuwa alikuwa akimpenda Peter,” aliongeza.

Hata hivyo, mapacha hao wa P-Square wameongea na inaonekana amani imerudi Squareville. Weekend hii Peter na Paul wametumia mtandao wa Twitter kueleza msimamo wa kundi lao na kwamba halijavunjika na haliwezi kuvunjika kamwe. Paul anayetumia ‏@rudeboypsquare kwenye Twitter ameandika: PSQUARE! Stronger than Ever!!! na Peter anayetumia jina ‏@PeterPsquare akiandika: FOREVER PSQUARE!

Awali, Peter alidaiwa kugoma kuondoa kinyongo chake kwa kaka zake akiwemo Paul licha ya kuombwa sana marafiki zake.

Pacha huyo alisema kama familia inataka kuwa na amani ni lazima imkubali na kumheshimu mke wake Lola. “Peter amechoka kutokana na kutumia miaka mingi kuiomba familia yake imkubali mwanamke aliyeamua kumuoa. Anataka Lola akubalike kwenye familia kama Anita (mke wa Paul) alivyokubalika bila kuzingatia utofauti wa umri wao,” chanzo kilicho karibu na familia hiyo kililiambia gazeti Vanguard.

Paul-Okoye-and-Anita-Isamas-pre-wedding-shoot-5-600x387
Paul na mkewe Anita

Vyanzo vilisema kuwa ugomvi wao ulikuwa mkubwa zaidi baada ya kubainika kuwa Peter amemnunulia nyumba Lola nchini Marekani.

Vanguard limedai kuwa kwa sasa Paul na Peter wameanza kuongea tena japo Paul hajaonesha kukubali ombi la pacha wake kwakuwa hata mama yao kabla hajafa alikuwa hajakubali uhusiano wa Peter na Lola.

Katika hatua nyingine Kaka yao Jude Okoye ambaye anadaiwa kuwa na mchango mkubwa wa ugomvi wa Peter na Paul, alitweet kueleza kuwa kwake familia ni kitu cha kwanza na kwamba P-Square itadumu.

Sababu za ugomvi baina ya mapacha wa P-Square zafahamika (details)

Alhamis hii alitweet:

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents