Burudani

Kala: Hatutaki watu wa kati kwenye show za makampuni

Kala Jeremiah amefunguka kuhusu yale yanayomkwaza moyoni kuhusiana na muziki wa Tanzania ulipofika.

Kala Jeremah

Rapper huyo ameoeneshwa kukerwa na kuendelea kuona wasanii wengi wakiwa maskini kwasababu ya watu wachache wanaohodhi kila kitu.

“Kwa ninavyofahamu mimi biashara ya muziki ni biashara kubwa sana na inayoweza kumtoa mhusika kwenye zero na kumpeleka kwenye hero kwa muda wa mwezi mmoja tu, je kwa nini wasanii wabongo hatuna hela,” amehoji Kala kwenye Instagram.

“Nikisema hatuna hela namaanisha wote hatuna hela. Je ni kweli tunahitaji kujitangaza kimataifa ndiyo tupate hela? Je ni kweli soko letu la ndani halitoshi kutupa mafanikio? Mimi nimefanikiwa kuishi nchini Uganda wasanii wa uganda wana mafanikio makubwa sana ya kifedha na kiuchumi na hawategemei soko la nje bali soko la ndani ya nchi yao tu. na mbaya zaidi nchi yao ni ndogo sana ukilinganisha na li nchi letu kuubwa,” ameongeza.

“Je kwa nini makampuni makubwa hayadili moja kwa moja na wasanii yanapowahitaji kwenye matamasha yao au kazi zingine yanatumia watu wa kati? Je makampuni yanajua kuwa watu wa kati wana wasanii wao??”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents