Burudani

Kala Jeremiah adai muziki umezima ndoto yake ya kwenda kucheza kikapu Marekani

Kala Jeremiah amesema muziki anaofanya umezima ndoto yake ya kwenda kucheza mpira wa kikapu katika ligi ya NBA nchini Marekani.

Kala

Akizungumza katika kipindi cha E-Newz cha EATV, Kala alisema, anaamini isingekuwa muziki angebakia katika upande wa mchezo huo anaouhusudu mpaka sasa. Amedai kwa sasa amebaki kama shabiki tu na anacheza mchezo huo kwa kujifurahisha tu mtaani.

Kala aliyeachia video ya wimbo Malkia mwishoni mwa mwaka jana ameeleza pia kuwa timu ya NBA anayoikubali ni Los Angeles Lakers huku akimkubali zaidi Kobe Bryant.

Hivi karibuni Bryant alitangaza atastaaafu mchezo huo baada ya kumalizika kwa msimu unaoendelea.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents