Burudani

Kala Jeremiah atangaza kumpata marehemu Ngwair tuzo ya msanii bora wa Hip Hop, ataipeleka Morogoro

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, mshindi wa tuzo tatu za KTMA 2013, Kala Jeremiah ametangaza kuwa tuzo ya Msanii bora wa Hip Hop ameamua kumpa marehemu Albert Mangwea.

IMG_4278-Copy

“Mimi kama msanii bora wa hip hop kwa mwaka huu napenda kuchukua muda huu kuwatangazia watu woote kuwa katika tuzo tatu nilizochukua moja naikabidhi kwa Albert Mangwea, yaani ni tuzo ya Mangwea na nitaipeleka kwa mama mzazi wa Mangwea, Morogoro,” ameandika.

“Nimeamua hayo kwa kuwa hayati Albert Mangwea alikuwa anafanya mziki ambao uko upande ambao mimi nimeshinda tuzo tatu yani hip hop.Tuzo niliyoamua kumpa mangwea ni tuzo ya msanii bora wa hip hop. kwa kuwa alikuwa anastahili pia kuitwa hivyo.

Tuzo hii naamini itakuwa ukumbusho mhimu sana kwa familia yake.lakini pia itakuwa inaonyesha mshikamano wetu kama wasanii wa hip hop, popote ulipo kama wewe ni shabiki wa hip hop tafuta njia yoyote ya kuendelea kumuenzi ndugu yetu.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents