Burudani

Kala Jeremiah: Nitagombea ubunge au urais miaka 10 ijayo

Rapper Kala Jeremiah amesema atafikiria kugombea nafasi ya ubunge au urais baada ya miaka 10 licha ya kushauriwa na watu mbalimbali kufanya hivyo muda huu.

Kala Jeremah

Kala ameiambia Bongo5 kuwa kwa sasa bado anataka kuendelea kuwatumikia wananchi kwa njia ya muziki.

“Mimi nimekuwa kati ya wasanii ambao nimekuwa nikishauriwa kuingia kwenye siasa na kugombea,” amesema rapper huyo. “Hiyo inamaanisha kuwa wameona nini ninachofanya kwenye muziki wangu. Na miaka ya nyuma viongozi walikuwa wanashauriwa, watu wanawaona kwanza, ndo ambacho kinatokea sana kwangu. Watu wananiomba nifanye hivyo ili niweze kuwatetea zaidi,” ameongeza.

“Mimi binafsi nimekuwa mbunge wa kujitegemea kwa miaka mingi ndio maana hata kazi zangu lazima nizungumze na watanzania kuhusu mambo mbalimbali. Ndio maana nikasema suala la kuingia kwenye siasa moja kwa moja mimi naona bado kidogo naona bado watu wananihitaji kwenye jukwaa la muziki. Ukifika wakati nina vipaumbele vingi sana.

Kama nikiwa mbunge nitaangalia changamoto za jimbo langu. Sasa kwa mfano nikiwa kiongozi mkuu wa nchi, tuchukulie urais kwa sababu ndani ya miaka kumi nitakuwa na uwezo wa kugombea urais kutokana na umri wangu unaweza kuruhusu. Kwahiyo nisipopita kwenye ubunge nikapita moja kwa moja kwenye urais, nitaanza kujenga Tanzania kwenye misingi iliyoachwa na vingozi wetu.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents