Habari

Kalamu ya digital inayohakiki na kutoa ishara ya makosa ‘spelling errors’ wakati wa kuandika kwa ku vibrate (video)

Wanasayansi usiku na mchana hawalali na kila kukicha wanazidi kuvumbua vitu vipya, sasa wamebuni kalamu ya digital inayoweza kua msaidizi wa mwandishi pale anapopitiwa na kufanya makosa madogo kama ya herufi na kutoa ishara.

pen

Wavumbuzi wa Ujerumani Falk Wolsky na Daniel Kaesmacher wamebuni kalamu ya digital yenye uwezo wa kubaini makosa ya herufi wakati wa kuandika na kumpa ishara anayeitumia.

Kalamu hiyo iliyopewa jina la kijerumani ‘Lernstift’ ,yenye maana ya kalamu ya kujifunzia ‘learning pen’, ina ‘built-in sensor’ yenye uwezo wa kutambua kile kinachoandikwa na kubaini muundo wa kila herufi hivyo kosa linapofanyika ina vibrate kumpa ishara anayeandika, kama ambavyo computer huchora mstari mwekundu kwenye neno lililokosewa herufi.

pen-2

Kalamu ya Lernstift pia ina Wi-Fi iliyojengewa ndani yenye uwezo wa ku connect na smartphone au PC na ku upload kwenye mtandao yale yaliyoandikwa kwenye karatasi kwa kutumia kalamu hiyo na kuweza kushare kwenye mitandao ya kijamii au sehemu yoyote. Mfano unaweza kuandika status yako ya facebook kwenye daftari au karatasi kwa kutumia kalamu ya Lernstift kisha ukaiweka kwenye akaunti yako ya facebook kwa njia hiyo bila kutype kwa computer au simu.

pen-3

Wabunifu wa kalamu hii Falk Wolsky na Daniel Kaesmacher wamesema hapo baadaye watakuja na model nyingine ambayo itakuwa na uwezo wa kusahihisha makosa ya grammar.

Wazo la kalamu hii lilitoka kwa mke wa Wolsky alipokuwa anamsaidia mtoto wao kufanya homework ndipo mume wake alilichukua na kuanza kulifanyia kazi.

Tazama video jinsi kalamu hiyo inavyofanya kazi

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents