Habari

Kalapina adai akikosa ‘Kitu cha Arusha’ chakula hakipandi

Msanii wa Hip Hop kutoka kikosi cha Mizinga Kalapina amesema amekuwa akishindwa kula na kufanya shughuli zake za kawaida pale anapokosa kitu cha Arusha aka ganja.

Karapina_peke_yake

Akiongea na chanzo chetu, Kalapina amesema amekuwa akipata shida anapokosa nafasi yakutumia mjani hali inayomsababishia kushindwa kula na kufanya mambo mengine kutokana na kushindwa kupata ari ya kufanya mambo bila nguvu ya mmea huo.

“Nimekuwa nikishindwa kula kwasababu ya kukosa kumtumia mjani, kitu ambacho kinanipa ari ya kufanya mambo mengi sana,” alisema.

Pia Kalapina amesema amekuwa akipata shida sana pindi anapotapa safari ambazo ndani yake kuna watu anaowaheshimu nakushindwa kupata nafasi ya kuvuta lakini akasema akizidiwa zaidi uzalendo humshinda na hivyo huvuta tu ili akae sawa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents