Habari

Kallaghe akana kumtapeli Kekuu


Mpiga picha wa Kampuni ya Kallaghe pictures John Kallaghe amesema yeye hajamtapeli msanii wa kike wa hip hop kutoka Arusha,Kekuu kama alivyotamka anavyodai.
Akizungumza na kituo cha Radio clouds fm katika kipindi cha xxl leo mchana mpiga picha huyo alisema anasikitishwa na hatua ya msanii huyo kumchukulia RB, kwani yeye alifanya kumsaidia msanii huyo katika kazi hiyo kwa kumpunguzia bei ambapo hata hivyo msanii huyo ameshindwa kulipa jumla ya kiasi walichokubaliana.
Akiendelea Kallaghe alisema “Mimi nilielewana nae kuhusu video yake miezi 6 iliyopita,na kwamba tulikubaliana anilipe shillingi laki 500,000 kitu ambacho alifanya kwa kunipa pesa 300,000 kama advansi na kisha ameshindwa kulipa pesa iliyobaki kwa wakati. Nilipo ona hakuna mwelekeo wa kulipwa pesa mi nikasimamisha kazi”.
Akimalizia Kallaghe anasema video hiyo bado anayo na msanii huyo anaonekana kutumia njia mbadala ili apate video bila malipo kamili.

Inavyosemekana msanii huyo wa kike wa hip hop kutoka jiji la Arusha amefungua jalada la Kesi dhidi ya mpiga picha wa Kampuni ya Kalaghe Pictures Bw. Kallaghe kwa kuwa amemtapeli pesa yake ya kushuti kideo na ni miezi 6 sasa anamtafuta hampati ikiwemo kutopokea simu zake wala kujibu sms.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents