BurudaniDiamond Platnumz

Kama Akifa Kesho: Huyu ndiye msanii Diamond anaamini ataipeperusha bendera ya Tanzania

Kuna mtu mmoja muhimu kwenye muziki aliwahi kunipigia simu na kuniuliza swali hili.. Hivi kama Diamond Platnumz bahati mbaya Mungu akimchukua, ni msanii gani mwingine wa Tanzania anayeweza kufanya anachokifanya yeye kwa sasa na jinsi anavyoitangaza Tanzania?’ Sikumbuki nilimpa jibu gani.. lakini Diamond Platnumz anaweza kuwa na jibu zuri kwa mtu huyu.

7cf829e4a60511e3a5b712a3de486cc5_8

“Moja ya watu ambao naamini hata NIKIFA kesho, Roho yangu itakuwa na amani ya kuamini kwamba kuna mtu ambae anaipeperusha vyema bendera ya Nchi yangu kupitia muziki… you jus call him @ommydimpoz ila wacha mi nimuite Kibonde,” Diamond ameandika kwenye Instagram kwenye picha ya Ommy akiwa amesimama pembeni ya gari la kifahari aina ya Lamborghini wakati akishoot video ya wimbo wake mpya na muongozaji maarufu wa video Afrika, Moe Musa.

IMG-20140307-WA0001

Unaizungumziaje kauli ya Diamond?

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents