Burudani

Kama mnaona tumekonda, leteni show tunenepe – Ruby

Msanii wa muziki Bongo, Ruby amefunguka kuhusu stori zinazodai kwa sasa mwili wake umepungua (amekonda) ukilinganisha na hapo awali.

Muimbaji huyo anayetamba na ngoma ‘Niwaze’ ameiambia FNL ya EATV kuwa picha zilizokuwa zikisambaa kwenye mitandao hajui zimetokea wapi.

Ruby alienda mbali zaidi kwa kueleza kuwa picha hizo zimefanyiwa editing na wale wanaoeneza stori hilo wampe kazi (show) ili anenepe.

“Halafu kitu kingine basi wawe wanaleta shows, kazi ili tunenepe, hivyo ndio vitu vya kuongea. Kama mnaona tumekonda, mnataka tunenepe, mnaleta shows, kazi,” amesema Ruby.

Ruby alikuwa kimya kwa kipindi kirefu katika muziki mara baada ya kuzinguana na menejimenti yake ya zamani. Wimbo wa kwanza kutoa kwa mwaka huu ni Niwaze aliowashirikisha kundi la The Mafik.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents