Mitindo

Kama unamtaka Hamisa Mobeto awe ‘video queen’ kwenye video yako jipange hivi

Mwanamitindo Hamisa Mobeto amefunguka na kueleza vigezo ambavyo anavihiitaji ili aweze kuonekana kwenye video yako ya muziki kwa sasa.

Mobeto

Akizungumza na Bongo5 Jumatatu hii, Hamisa alisema pesa siyo kigezo kikuu ili ashiriki kwenye video yako.

“Kwa sasa sitaki kufanya video lakini kama wakitokea watu wakanilipa vizuri nitafanya,” alisema Hamisa. “Kama tutakubaliana kufanya video na mtu, nitaanza kuusikiliza wimbo kwanza, pia unatakiwa unilipe vizuri kwa sababu mimi ni brand, nakuja kwenye kazi yako ili kuongeza thamani, kwa hiyo acha ninufaike na brand yangu,”

Mrembo huyo ambaye aliwahi kuonekana kwenye video kadhaa kama video ya wimbo ‘My baby’ ya Quick Rocka, amesema swala la bei anazotoza zinategemeana na msanii na aina ya wimbo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents