Kama wewe ni Blogger au unaendesha channel ya YouTube, usipitwe na kauli hii ya Waziri Mwakyembe (+video)

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amewatangazia habari nzuri watu wote wanaoendesha huduma ya za kutoa habari mitandaoni ikwemo Mabloggers na waendeshaji wa channel za YouTube.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Julai 06, 2018 Jijini Dar es salaam, Mwakyembe amesema kuwa yupo tayari kukaa na kundi hilo la watoa huduma ya habari mitandaoni ili kuangalia gharama za kulipia leseni ambayo inazidi kiasi cha shilingi milioni 1.

Mwakyembe amesema atakaa na jopo la wanasheria kutoka TCRA ili kuangalia namna ya kupunguza gharama za kupata leseni.

 

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW