Fahamu

Kama wewe ni Mjasiriamali na Mfanyabiashara mdogo unayetaka kutoboa, taarifa hii nzuri ikufikie

Mafunzo ya awamu ya tatu ya mfululizo wa mradi wa ‘Founder to Founders’ yamefanyika leo jijini Dar Es Salaam, katika ofisi za Seedspace, Victoria.

Baadhi ya washiriki wa jukwaa la Founder 2 Founders iliyoandaliwa na SmartLab wakifurahia kupata selfie ya kumbukumbu baada ya kongamano hilo kumalizika.


Mafunzo hayo yanayosimamiwa na Smartlab, yamekua yakileta pamoja watu kwenye sekta ya uvumbuzi kwa maongezi na kufundishana miongoni mwa hao waanzilishi.

Kutoka wa pili kushoto ni Kumeil Abdulrasul, bidhaa na masuala ya ushirikiano kutoka Raha Liquid Telecom, Edwin Bruno, mwanzilishi wa Smartcodes na SmartLab, rais wa chuo cha St. Joseph, Stanley Kafu, msimamizi mkuu wa masoko kutoka benki ya Exim. Kwa pamoja wakiwa katika tukio la Founder To Founders .

Smartlab wanafanya hivyo kupitia majadiliano kwenye mada tofauti tofauti ili kupata ufahamu wa jinsi ya kukuza kampuni mpya. Tukio lilikua na mandhari ya “Jinsi ya kukuza kiufanisi soko la kampuni yako mpya” na ilikua na jopo la watu kutoka sekta tofauti tofauti.


Meneja Mradi wa SmartLab, Juliana Kayombo (wa pili kulia) akifafanua jambo katika mkutano huo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.


Mwanzilishi kwa Waanzilishi ni jukwaa kwa ajili ya kampuni mpya kukutana na wawekezaji, waanzilishi wenza na washirika.

Na inawawezesha kuungana na kushirikiana wakati wa kubadilishana mawazo ya ubunifu kwa ajili ya kukua, kubadilisha mitazamo na kutengeneza ufumbuzi wa kubadilisha mazingira ya Tanzania na Afrika kwa ujumla.

Baadhi ya washiriki wa jukwaa la Founder 2 Founders iliyoandaliwa na SmartLab wakifuatilia kwa ukaribu tukio hilo


Akiongea kwenye tukio, Edwin Bruno, Mwanzilishi wa SmartLab na mkurugenzi mtendaji wa Smart codes Limited alisema kwamba “Kampuni mpya, wajasiriamali, wabunifu na wavumbuzi wa biashara za hapa nyumbani sasa wana sehemu moja ya kukutana na kufanya shughuli ambazo zitakutanisha na kukuza jumuiya za uvumbuzi zilizo tofauti na zenye vipaji hapa Tanzania na afrika kwa ujumla kupitia Mwanzilishi kwa Waanzilishi”, Pia alieleza kua “Jukwaa la Mwanzilishi kwa Waanzilishi linatoa muungano wa muhimu ambao unawezesha wajasiriamali na kampuni mpya kujua mienendo mipya kwenye sekta ya uvumbuzi. Pia inawapa uwezo wa kujielezea kuhusu changamoto zao na hivyo kutengeneza nafasi za suluhisho kwa ajili ya mapungufu yao”.

Wadau wakifuatilia kwa ukaribu tukio hilo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents