Habari

Kamanda Mambosasa afunguka kifo cha mtu mmoja aliyepigwa risasi na polisi

Wakati wananchi katika mitandao ya kijamii wakiendea kutuma picha mitandaoni za binti aliyepigwa risasi kwa majonzi, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amekiri mtu mmoja kupigwa risasi na polisi wakati wakiwatawanya wafuasi wa Chadema walioandama jana Februari 16, 2018.

Binti aliyedaiwa kupigwa risasi na jeshi la polisi

Wafuasi hao wa Chadema wakiongozwa na mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe waliandamana kuelekea ofisi ya msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Kinondoni, Aron Kagurumjuli kudai viapo vya mawakala wa chama hicho.

Maandamano hayo yalianzia viwanja vya Buibui Mwananyamala ulikokuwa ukifanyika mkutano wa kampeni wa Chadema na yalipofika eneo la Mkwajuni wafuasi hao walitawanywa na polisi, huku mtu mmoja aliyekuwa kwenye basi la daladala akidaiwa kupigwa risasi na kufariki dunia.

Akizungumza na Mwananchi, Jumamosi hii, Mambosasa amesema “Walizuia mwendo kasi, wakaanza kupiga mawe kwa hiyo kati ya risasi za hewani zilizopigwa kuwatawanya kuna iliyompata (mtu).”

Ufafanuzi huo wa Mambosasa licha ya kutoweka wazi kama mtu huyo amefariki dunia ama la, umekuja huku ikidaiwa kuwa aliyepigwa risasi na kupoteza maisha ni mwanafunzi wa elimu ya juu.

Taarifa za kifo cha mwanafunzi huyo zilianza kusambaa tangu Ijumaa jioni katika mitandao ya kijamii sambamba na kuwekwa picha yake huku ikieleza kuwa amepigwa risasi wakati akiteremka katika basi.

Mambosasa alipoulizwa kama mtu huyo ni mwanafunzi wa elimu ya juu amesema, “Haijathibitishwa hiyo, nipo kwenye pilika za uchaguzi, nadhani nitajibu hilo nitakaporejea ofisini na kupata taarifa.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents