Habari

Kamanda Mpinga, RPC mpya mkoa wa Mbeya

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Saimon Sirro, amefanya mabadiliko ya Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga pamoja na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya Dhahiri Kidavashari.

Katika mabadiliko hayo, aliyekuwa Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Naibu Kamishna wa Polisi Mohamed Mpinga anaenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, na nafasi yake inachukuliwa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Fortunatus Musilimu.

Aidha, Aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya (DCP) Dhahiri Kidavashari amehamishiwa Makao Makuu ya Upelelezi.

Uhamisho huo ni wa kawaida katika kuboresha utendaji wa kazi za Polisi kwa mujibu wa kanuni, taratibu na miongozo ya Jeshi la Polisi.

Imetolewa na:
Barnabas D. Mwakalukwa – ACP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Makao Makuu ya Jeshi la Polisi.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents