Habari

Kamati ya Bunge yamsamehe Lowassa

MWENYEKITI wa Kamati Teule ya Bunge ya Kuchunguza Mchakato wa Zabuni ya Kuzalisha Umeme wa Dharura ulioipa ushindi Kampuni ya Richmond Development, Dk Harrison Mwakyembe amesema kamati yake imesamehe matamshi ya Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa kwamba ilisema uwongo kwa kumhusisha na kashfa ya Richmond.

Na Midraj Ibrahim, Dodoma

 

 

 

MWENYEKITI wa Kamati Teule ya Bunge ya Kuchunguza Mchakato wa Zabuni ya Kuzalisha Umeme wa Dharura ulioipa ushindi Kampuni ya Richmond Development, Dk Harrison Mwakyembe amesema kamati yake imesamehe matamshi ya Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa kwamba ilisema uwongo kwa kumhusisha na kashfa ya Richmond.

 

 

 

Akifanya majumuisho ya hoja ya kamati yake, Dk Mwakyembe alisisitiza kuwa kamati yake ilifanya kazi kwa umakini na taarifa yake ni sahihi na kweli, tofuati na alivyosema Lowassa wakati wa kutoa hoja yake bungeni baada ya taarifa hiyo, ambayo ilimhusisha kwenye kashfa hiyo kwa kushinikiza Richmond ipewa zabuni, akiwa Waziri Mkuu wa Tanzania na hatimaye kutangaza kujiuzulu.

 

 

 

Alisema kamati imeamua kumsamamehe Lowassa ili kupisha kuendeleza malumbano yasiyo na maana na kwamba wanajua kwamba huoenda alisema hayo kwa hasira.

 

 

 

Dk Mwakyembe alilifahamisha Bunge kwamba kamati yake haikuwa na shida ya cheo chake cha uwaziri mkuu , bali walifanya kazi ili kuweka wazi hali waliyikuta kwenye uchunguzi wao na kwamba hawakuona umuhimu wa kumhoji Waziri Mkuu kwa kuwa baadhi ya mawasiliano kati yake na Waziri wa Nishati na Madini kuhusiana na jambo hilo zilijitosheleza.

 

 

 

Alisema hata hivyo katika mapendekezo ya kamati hawakusema waziri Mkuu awajibishwe kama ilivyo kwa wahusika wengine bali walisema yeye mwenyewe apime kulingana na tuhuma hizo ambazo zilimhusisha kwenye sakata hilo kupitia kwa watendaji wake wa chini.

 

 

 

Kuhusu Lowassa kujiuzulu Uwaziri Mkuu, Dk Mwakyembe alisema hata kama hakuhusika moja kwa moja na suala hilo, alistahili kwa sababu amewajibika kwa makosa ya watu walio chini yake.

 

 

 

Wakati akitangaza kujiuzulu wadhifa wake bungeni wiki iliyopita, Lowassa aliituhumu kamati hiyo kushindwa kumhoji ilhali ofisi za Bunge ziko mita chach kutoka ofisini kwake na kwamba baada ya kutafakari alibaini tatizo ni Uwaziri Mkuu.

 

 

 

Dk Mwakyembe alisema fursa ya Lowassa kujieleza ilikuwepo, bali hakutaka kuitumia pale alipopewa nafasi ya kwanza kuchangia ripoti hiyo, badala yake alielekeza kumshambulia yeye na kamati yake.

 

 

 

Hivi ulishawahi kusikia mtu analalamika kuwa polisi hawakumpa nafasi ya kusikilizwa?� alihoji Dk Mwakyembe.

 

 

 

Alisema kamati yake ilitoa mataangazo na kuomba watu wenye ushahidi kujitokeza, lakini Lowassa hakutaka akasubiri afuatwe badala yake, analalamikia haki ya kusikilizwa.

 

 

 

Awali, Dk Mwakyembe alisema kwenye ripoti hiyo hakuna inakomtaja Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz kuwa ni mmiliki wa Richmond.

 

 

 

Source: Mwananchi

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents