Michezo

Kamati ya katiba, sheria za wachezaji kutoa hukumu ya Kessy Septemba 4

Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji Jumapili ya Septemba 4, 2016 inatarajiwa kutoa hukumu ya beki wa Yanga Hassan Ramadhan ‘Kessy’ anayedaiwa na Klabu ya Simba kuvunja mkataba kwa kuanza kufanya mazoezi na klabu ya hiyo aliyojiunga nayo hivi karibuni.

kessy-hassan-ramadhan_w1l3hhf7te9d19mb1h0h17qdr

Uongozi wa klabu ya Simba kupitia kwa Msemaji wake Hajji Manara wameiambia Goal, hawatakubali kuona mchezaji huyo akiendelea kuichezea Yanga kwani amevunja vipengele muhimu kwenye mkataba baina yake na Simba.

“Tumewasilisha vielelezo vyote vya msingi ambavyo vinatupasa kuvisimamia ili kupta haki yetu kutoka kwa Kesssy na ninaamini Kamati itatutendea haki hiyo Jumapili,” amesema Manara.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamati hiyo, shauri hilo lilisikilizwa na uamuzi wake utatolewa Jumapili ijayo, hiyo ni baada ya kushindikana kusikilizwa kwa shauri jingine linalohusu klabu Simba ikiilalamikia Yanga, kuingia mkataba na mchezaji Hassan Ramadhani Kessy wakati bado ana mkataba na klabu Simba.

Shauri hilo lilishindikana kusikilizwa wiki iliyopita kwa sababu viongozi wa Yanga hawakutokea mbele ya kamati hiyo wakati wa kusikiliza shauri hilo, hivyo kamati itaiandikia barua Yanga kukumbushwa kuhudhuria kwenye kesi hiyo Jumapili ijayo kabla ya kutolewa uamuzi.

Source: Goal

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents