Michezo

Kamati ya Rufaa ya TFF yawashushia rungu zito Ditopile na Chibula

Kamati ya Rufaa ya Maadili ya TFF, imeitupilia mbali rufaa ya Dustan Mkundi Ditopile na kuiagiza Sekretariati kulipeleka suala Lake katia vyombo vya ulinzi kwa uchunguzi zaidi.

Dustan alifungiwa kutokana na kuwasilisha fomu ya mapato tofauti na fomu halisi ya Bodi ya Ligi.

Wakati huo huo kamati hiyo imesema Edgar Chibula ambaye ni Mwenyekiti wa Abajalo FC na Mjumbe wa Bodi ya Ligi alikiri kutoa maneno makali mbele ya vyombo vya habari akiwa kama kiongozi.

Kutokana na kukubali kwake kwa kosa hilo kamati ya Rufaa na Maadili imemfungulia kifungo cha kutojihusisha na soka kiongozi huyo pamoja na kumpa onyo kali.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents