Michezo

Kamati ya zabuni ya Simba SC kuzungumza kesho

Kamati maalumu ya kusimamia mchakato wa zabuni ya kumpata muwekezaji kwenyemuundo mpya wa klabu ya Simba inatarajia kuzungumzia maendeleo yake kesho siku ya Jumamosi.

Simba SC ilipitisha maamuzi ya kubadilisha umiliki wake kutoka klabu ya michezo inayomilikiwa na wanachama na kuwa kampuni inayomilikiwa na wanahisa.

Simba SC yatangaza kamati ya kusimamia mchakato wa zabuni

Kamati ya utendaji ya klabu hiyo iliamua kuunda kamati ya kupitia mchakato wa zabuni wa kumpata mwekezaji au wawekezaji ambao ni wanachama wa Simba, watakaonunua hadi asilimia 50 ya hisa za klabu ya Simba.

Katika asilimia 100, asilimia 50 zitauzwa kwa mwanachama wa Simba kwa mfumo wa tenda ambao mchakato huo unasimamiwa na kamati hiyo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents