Habari

Kampeni ya ‘Mti wangu’ kufanyika wikiendi hii

Kampeni ya ‘Mti Wangu’ ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, itafanyika Jumamosi hii, Oktoba 1.

14294852_1802251463389472_508673264_n

Makonda amewataka wakazi wa Dar es Salaam kuiunga mkono kampeni hiyo.

03

“Faida za miti zipo nyingi sana, tunaamini kwa kipindi hiki tutafikia malengo ambayo tumekuwa tukiyafikiria,” alisema Makonda wakati akiwa katika msafara wake wa zoezi la ukaguzi wa upandaji miti akiongozana na mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Ally Salum Hapi.

“Nimshukuru mkuu wa mkoa wa Kinondoni kwa kazi nzuri ambayo ameendelea kuifanya kuniunga mkono, akishirikiana na mkurugenzi wake na wadau wengine na wataalamu wote, kuhakikisha kile ambacho wanaelekezwa wanakifanya kwa uaminifu na kuongeza ubunifu unaoweza kuongeza thamani,” aliongeza.

Pia aliwashukuru watu na makampuni yote yanayomuunga mkono.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents