Michezo

Kampeni za TFF: Mulamu ajinadi kukuza mapato na kuinua soka la vijana (+Video)

Kuelekea Agosti 12 mwaka huu katika uchaguzi mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) hatimaye kampeni za uchaguzi huo zazinduliwa rasmi leo.

Akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa kampezni yake Mulamu Erick Nghambi anayewania nafasi ya Makamu wa Rais wa TFF, ameeleza kuwa anania ya dhati ya kufikisha soko la Tanzania mbele zaidi kwa kuhakikisha mapato yanaongezeka.

“Katika uongozi wangu kwa kushirikiana na Kamati ya Utendaji tutaboresha ofisi ili kuwafanya wafanyakazi na watendaji kufanya kazi zao katika mazingira mazuri na yakisasa, pia nitahakikisha mapato yanaongezeka nitashirikiana na Kamati ya Utendaji kwa kuweka mifumo ya mashine za kieletroniki kwenye uuzaji wa tiketi wakati wote nchi nzima ili kusaidia klabu kupata mapato pamoja na srikali,” amesema Maluma.

Pia amesisitiza ‘Katika uongzoi wangu nitahakikisha kuwa kila Mkoa unaendesha program ya kuendeleza vijana wenye chini ya umri wa miaka 13 kupitia shule za msingi na sekondari jkwa kushirikiana na TAMISEMI , vile vile kwa upande wa wanawake tutahakikisha soka lina imarika na kuanzisha utaratibu mahususi wa kupata wasichana wa kucheza mchezo huo na kuwapatia walimu na wakufunzi wa kike,” amesema Malamu.

Na Laila Sued na Salum Kaorata

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents