DStv Inogilee!

Kampeni zinafikia tamati, uchaguzi mkuu ni Jumapili hii, Chukua tahadhari

Wakati kampeni za wagombea kwenye kinyang’anyiro cha uraisi, wabunge na madiwani zikiendelea kila mtu akijaribu kujihakikishia kwa namna moja au nyingine anapata wapiga kura wengi zaidi ili aweze kushinda, kuna vitu vya hapa na pale kwa mtu mwenye uelewa unatakiwa kuwa makini navyo.

507c476363065.preview-620

Ingawa tumejaa na hisia mbalimbali kuhusu uchaguzi wa mwaka huu, kitu nilichojifunza ni kuchukua tahadhari za kimakusudi kabisa kwenye maeneo yafuatayo;

Epuka mazungumzo yenye mabishano, chuki na uhasama ndani yake

Kuna baadhi ya watu hawako kama vile unavyowafahamu, kuna hisia za namna mbalimbali kuhusu uchaguzi huu, wengine hawajali urafiki au mahusiano yao kabisa wako tayari kukufanya chochote au kusema vyovyote kwasababu ya itikadi zao kisiasa.

Hivyo kwa namna moja ama nyingine kama hauko makini utajikuta ukiingia kwenye ugomvi na mtu au watu wengine. Najua kuna watu wanapenda mabishano na kama mabishano yameshafanyika sana na kila mtu anajua nini cha kufanya kutokana na mwenendo mzima wa kampeni, hivyo haina sababu ya kuendelea kubishana na watu huku ukijiletea ugomvi usiokuwa na sababu. Kitu kingine kwanini unatakiwa kuepuka mabishano; watu wengi sasa wanaendeshwa na hisia hivyo wako tayari kuingia kwenye ugomvi kwasababu ya mtu fulani au itikadi fulani.

Hakuna mtu atakayeweza kukulinda kama huwezi kulinda maisha yako mwenyewe kutokana na kauli zako na mazungumzo gani unajihusisha nayo kwa wakati huu na siku chache hizi zilizobakia kupiga kura yako. Kuna Maisha baada ya uchaguzi, tahadhari ni muhimu sana.

Jipange
Siku moja au mbili kabla ya uchaguzi, nakushauri kuwa, nunua vitu vya msingi vya matumizi yako ya ndani hasa vyakula ili siku ya kupiga kura na wakati watu wanasubiri matokeo si watu wote wenye ujasiri wa kufungua biashara zao. Unahitaji akiba ya chakula cha kutosha, usije unajikuta unalala njaa kwa ujinga wako tu binafsi. Kitu kingine vitu vinaweza kupanda bei bila sababu yoyote au kwasababu wengine wataogopa kufungua biashara zao hivyo wale wachache watakaoweza kufungua biashara hizo wanaweza kutumia fursa hiyo kujipatia faida mara dufu.

Wewe na familia yako kupunguza mizunguko isiyokuwa ya msingi

Watu wengi huwa wanajitahidi kuepuka vurugu za hapa na pale, wewe na familia yako msizurule ovyo kwani mnaweza mkakutana na watu katika kampeni zao na kwasababu moja ama nyingine kuna baadhi ya makundi ambayo kampeni na vurugu kwao ni fursa ya kujipatia chochote. Watu wanasema akili yako iwe macho kujua na kutambua nyakati ulizopo na mabo ya kuyaepuka.

Kuna watu hiki ni kipindi cha biashara kwao

Ninaposema kuchukua tahadhari kuna watu wengine hiki ni kipindi cha biashara kwao, yaani uchaguzi, siasa na kampeni ni wakati wa kukusanya mapato kwa njia moja ama nyingine hivyo unaweza ukajikuta unatumika bila ya wewe kujijua. Usiruhusu wewe kuwa chambo ya jambo lolote akili ni nywele kila mtu ana zake, kuwa makini. Zaidi ya yote tuombe Mungu kuwe na amani, utulivu na kutulia wakati wote wa kupiga kura na washindi wanapotangazwa.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW