Habari

Apple Inc kuja na TV inayoweza kuruka matangazo, na inayotumia remote ya pete inayovaliwa kidoleni na mtazamaji

Ndoto za Steve Jobs zinazidi kuendelezwa hata baada ya yeye kufariki (October 5, 2011). Baada ya kufanya vizuri katika ulimwengu wa computer na smart phones (iphone) ambazo zimeleta ushindani mkubwa sokoni, sasa kampuni ya Apple Inc inakuja na ‘TV set’ ambayo mtazamaji atakuwa na uwezo wa kuruka matangazo ya biashara wakati wa kutazama, na pia itakuwa na remote ya pete itakayokuwa inavaliwa kidoleni na mtazamaji.

Apple

Kampuni ya Apple Inc iliyoanzishwa (April 1, 1976) imetangaza kuwa baadaye mwaka huu itazindua TV hiyo ambayo pia itamuwezesha mtazamaji kuruka matangazo ya biashara wakati anatazama vipindi anavyovipenda kama ilivyoripotiwa na Daily maily.

Kampuni hiyo ya Apple imesema iko katika majadiliano na vituo vya televisheni na pia wako tayari kuwafidia mapato watakayopoteza ili kuwawezesha watazamaji watakaonunua TV hizo wawe huru kuangalia vipindi (vilivyorekodiwa) bila usumbufu wa matangazo ya biashara, hii ikiwa njia ya kuvuta wateja wengi zaidi katika bidhaa yao mpya ya TV.

Hata hivyo vyanzo vimesema huduma hiyo ya kuruka matangazo haitakuwa ikitumika katika vipindi vya Live.

Kitu kingine kuhusiana na TV hiyo mpya ya Apple, inasemekana itakuwa ina remote ya pete (iring) itakayokuwa inavaliwa na mtu anayetazama na kuweza kubadilisha channel, kuongeza sauti na vitu vingine kwa kutumia pete hiyo.

Yanko Design ndio wamehusika kubuni picha za jinsi ambavyo pete hiyo na TV set vitakavyoonekana.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents