Uncategorized

Kampuni ya Boeing yasitisha matumizi ya ndege zote za 737 Max, ni baada ya kuanguka ndege ya Ethiopia Airlines

Kampuni ya Boeing Marekani inayotengeneza ndege iliyoanguka Ethiopia imesitisha matumizi ya ndege zote aina hiyo baada ya wachunguzi kubaini ushahidi mpya katika eneo ambako ndege ya Ethiopia Airlines ilianguka.

Kwa mujibu wa sgirika la habari la BBC, Kampuni hiyo ya Marekani imesema itasitisha usafiri wa ndege zote 371 zinazohudumu.

Shirika linalosimamia usafiri wa anga Marekani FAA, limesema ushahidi mpya pamoja na data mpya za satelaiti zimechangia uamuzi huo wa kupiga marufuku kwa muda usafiri wa ndege hizo.

FAA awali lilisisitiza ndege ya Boeing 737 Max 8 ni salama wakati mataifa mengine yakipiga marufuku usafiri wa ndege hizo.

Ajali hiyo siku ya Jumapili mjini Addis Ababa ulisababisha vifo vya watu 157.

Personal belongings from the Ethiopian Airlines plane crash on Sunday

Ni ajali ya pili kuwahi kushuhudiwa ya ndege hiyo chapa Max 8 katika miezi mitano baada ya ajali nyingine nchini Indonesia mwaka jana Oktoba iliosababisha vifo vya watu 189.

Shirika la FAA limegundua nini?

FAA lina kundi la maafisa wanaochunguza mkasa huo katika eneo ambapo ajali ya shirika la ndege la Ethiopia ilipotokea likishirikiana na bodi ya kitaifa ya usalama wa safari.

Dan Elwell, kaimu msimamizi katika shirika hilo FAA, amesema Jumatano: ” Imebainika wazi kwa pande zote kwamba safari ya ndege ya Ethiopia ilikaribiana na namna ilivyoshuhudiwa kwa ndege iliyoanguka awali ya Lion Air .”Marekani: Boeing 737 Max 8 ni salama

Ameongeza kwamba “ushahidi tuliopata katika eneo, umefanya kuwa na uwezekano mkubwa kwamba hata njia ya ndege ilikaribiana na ile ya Lion Air”.

Presentational grey line

Ruka ujumbe wa Twitter wa @FAANews

Boeing 737 Max

Rais Donald Trump awali alitangaza kwamba shirika la FAA litatoa tangazo la dharura kufuatia “taarifa mpya na ushahidi tuliopokea kutoka eneo la mkasa na kutoka maeneo mengine kupitia malalamiko mengine tofauti”.

Marekani ni nchi ya hivi karibuni kusitisha usafiri wa ndege hiyo ya Boeing 737 Max yakiwemo mataifa mengine kama Uingereza, Umoja wa Ulaya, China India na Australia ambayo yote yameamua kusitisha usafiri wa ndege hizo.

Kufikia leo, msimamo wa FAA ni kwamba ukaguzi umeonyesha ” hakuna matatizo ya mfumo wa utendaji kazi” na kwamba hakuna msingi wa kusitisha usafiri wa ndege hizo.

ramani Ethiopia airlines
ramani Ethiopia airlines

Kampuni ya Boeing imesema nini?

Boeing, mtengenezaji wa ndege hizo imesema “inaendelea kuwa na imani kubwa katika usalama wa ndege za 737 Max”.

Hatahivyo, limeongeza baada ya mashauriano na FAA na bodi ya taifa ya usalama wa safari kwamba imeamua kupiga marufuku safari za ndege hizo ” kutokana na kutambua umuhimu wa tahadhari na katika kutoa hakikisho kwa umma wanaotumia ndege kuhusu usalama wa ndege hizo”.Ibada ya mazishi ya rubani wa ndege ya Ethiopia Yared imefanyika

Ethiopian Airlines: Ni nani waliopoteza maisha?

Dennis Muilenburg, rais, mkurugenzi mtendaji na mwenyekiti wa Boeing, amesema: ” Tunafanya kila tuwezalo kuelewa chanzo cha ajali hizo na wachunguzi, tutatuma vifaa vya usalama zaidi na kuhakikisha kwamba hili halifanyiki tena.”

People gather at the Ethiopian Airline crash site

Sara Nelson, rais wa muungano wa wahudumu wa ndege -CWA, amesema: “Maisha ya watu siku zote ndio muhimu zaidi. Lakini hadhi ya bidhaa kuu ipo hatarini pia. Na bidhaa hiyo sio tu Boeing. Ni Marekani.”

Hisa za Boeing zimeongezeka juu hadi $377 kwa kila moja kufuatia tangazo hilo.

Hatahivyo, thamani ya kampuni hiyo katika soko imeshuka kwa takriban $26bn tangu kutokea mkasa wa ajali hiyo ya ndege ya Ethiopia siku ya Jumapili.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents