Technology

Kampuni ya Facebook yawaomba radhi watumiaji wa App zake za Instagram, WhatsApp na Facebook ”Tutarudi kwa asilimia 100”

Kampuni ya Facebook inayomiliki App zote tatu ambazo ni Facebook, Instagram, WhatsApp imewaomba radhi watumiaji wake kwa usumbufu uliyojitokeza hapo jana.

Nembo ya Facebook kwenye smartphone

Kupitia akaunti yake ya Twitter, kampuni hiyo ya Facebook imewaombaradhi kwa usumbufu huo ambao kulikuwa na ugumu wa kutuma, kupakua na kupokea picha na video hapo jana.

“Mapema leo, baadhi ya watu na wafanyabiashara walipata matatizo ya kupakia au kutuma picha, video na faili nyingine kwenye programu zetu na majukwaa. Suala hili limeshatatuliwa na tutarudi kwa asilimia 100% kwa kila mtu. Samahani kwa usumbufu wowote.”- Imesema Facebook

 

Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Kampuni ya Facebook inayomiliki App zote tatu, imesema inafahamu kuhusu tatizo hilo na ilikuwa ”ikifanyia kazi ili kurudisha kila kitu sawa haraka iwezekanavyo”.

 

 

 

Mitandao ya kijamii, ina mabilioni ya watumiaji wake ulimwenguni.

Washindani wake Twitter pia walikuwa na tatizo kwa watumiaji wake kushindwa kutuma ujumbe wa moja kwa moja au kupokea taarifa kuhusu ujumbe ulioingia.

Kampuni iliomba radhi kwa dosari hiyo kupitia ukurasa wake wa Twitter wakisema kuwa wanashughulikia tatizo hilo.

Watumiaji bado waliweza kuweka ujumbe kwenye twitter na ujumbe wa hashtag #instagramdown ukaanza kushika kasi mtandaoni wengi wakitumia kueleza matatizo ya mshindani wake.

App ya Facebook Messenger, ambayo huwa inapakuliwa kivyake, nayo ailiathirika.

Mwezi Machi, Facebook na Instagram ilipata changamoto za kiteknolojia ambayo ilidumu wa muda. Matatizo pia yalikumba app zote mbili sambamba na Whats App mwezi Aprili.

Facebook ina watumiaji zaidi ya bilioni 2.3 kwa mwezi wanaotumia app hiyo na Instagram ina watumiaji bilioni moja.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents