Burudani

Kampuni ya mavazi iliyoweka picha ya kibaguzi mtandaoni yaomba radhi

Kampuni ya mavazi ya H&M imeomba radhi kufutia picha ya tangazo la nguo kutafsiriwa kuwa la kibaguzi kwa mtu mweusi.

H&M ambayo imekuwa ikimvalisha msanii The Weeknd imetumia ukurasa wa mtandao wa wa kijamii wa Instagram kuimba radhi wadau na wapenzi wa mavazi kwa picha hiyo.

Barua ya kuomba radhi imeelezea kuwa kampuni  hawakuwa na nia mbaya kama ilivyo tafsiriwa na baadhi ya watu baada ya kijana huyo kuvaa T-Shirt iliyoandikwa “ Coolest Monkey In The Jungle” hata hivyo imesema kuwa watafanya uchunguzi kuhusu mtu aliye husika katika kuchapicha nguo hiyo.

Mpaka sasa kapuni hiyo imepoteza mkataba wake kwa mtayarishaji wa muziki na msanii wa muziki kutoka Canada The Weeknd baada ya picha hiyo kusambaa mitandaoni pia kampuni hiyo imejikuta ikishambuliwa katika mitandao ya kijamii.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents