Habari

Kampuni ya Steps Entertainment Limited leo kutoa tuzo 8 za Filamu Tanzania

Kampuni ya usambazaji wa filamu Tanzania ya Steps Entertainment Limited, leo itatoa tuzo kwa wasanii, Watayarishaji, Waongozaji na wadau mbalimbali waliopo katika tasnia ya filamu Tanzania. Shughuli ya utoaji wa tuzo hizo utafanyika kwenye Ukumbi wa Blue Pearl Ubungo Plaza kuanzia saa 1:00 usiku.

Meneja Masoko wa Steps Entertainment, Kambarage Ignnatus akionyesha moja ya tuzo zitakazotolewa kwa wasanii leo kwenye ukumbi wa Blue Pearl.
Meneja Masoko wa Steps Entertainment, Kambarage Ignnatus akionyesha moja ya tuzo zitakazotolewa kwa wasanii leo kwenye ukumbi wa Blue Pearl.

Tuzo ambazo zitatolewa usiku wa leo zitahusisha zaidi wasanii wanaofanya kazi na kampuni yao tu. Tuzo ambazo zinatarajiwa kutolewa ni pamoja na filamu bora ya mwaka, Kampuni iliyotengeneza filamu bora, msanii anayependwa na watu ndani na nje ya nchi, msanii bora chipukizi, mwigizaji bora wa kike, mwigizaji bora wa kiume, mwongozaji bora wa filamu na mwandishi bora wa filamu.

Mratibu wa tuzo hizo, Carlos Johns Silondwa amesema wameandaa tuzo hizo kwa lengo la kuleta ushindani na kukubali mchango wa wasanii, watayarishaji na wadau wote na pia ni kuwatambua na kujali mchango wa wasanii katika ukuzaji wa filamu nchini, ambapo tuzo hizo ni kichocheo kitakacholeta ushindani unaoweza kujenga tasnia ya filamu na kujenga ajira kwa jamii kubwa.

“Tunaamini kuwa tuzo zitakuwa kichocheo kikubwa cha kukuza tasnia ya filamu, kuongeza ushindani katika kutengeneza filamu bora, hadithi nzuri zinazoelimisha, kukuza na kuitangaza lugha ya Kiswahili nje ya mipaka ya Tanzania,” alisema Silondwa.

Source: Mwananchi

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents