Habari

Kampuni yanunua mji kwa ajili ya Bangi

Kampuni ya American Green, imekubali kununua mji wa Nipton uliopa jimbo la California Marekani ambao utakuwa kitovu cha bidhaa zilizo na kilevi aina ya Bangi.

Kampuni hiyo imenunua mji huo kwa kiasi cha dola milioni 5, wenye hekari 120 za ardhi ambazo zinajumuisha maeneo yenye shule, hoteli na duka kubwa. American Green wanatarajia kuwekeza hadi kiasi cha dola milioni 2.5, ilikuufufua mji huo ambao una wakazi 20 pekee.

Mji wa Nipton ulianzishwa wakati wa pilika pilika za kutafuta dhahabu karne ya 20, mji huo upo katika mpaka wa Hifadhi ya Taifa ya Mojave.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents