Michezo

Kamusoko avurugwa na suluhu ya Yanga dhidi ya Lipuli FC (Picha)

Pazia la Ligi kuu soka Tanzania Bara lilifunguliwa rasmi mapema tarehe 26 ya wikiendi iliyopita huku michezo kadhaa ikipigwa katika viwanja mbalimbali wakati kubwa ikiwa ni matokeo ya Yanga SC iliyocheza jana Jumapili dhidi ya timu iliyopanda daraja msimu huu wanapaluhengo, Lipuli FC.

Yanga inayodhaminiwa na kampuni ya kubashiri matokeo ya Sportpesa ilishuka uwanjani katika mchezo wake wa kwanza wa msimu wa mwaka 2017/18 kucheza na Lipuli FC ambayo nayo ikiwa ndiyo inarejea ligi kuu baada ya kukosekana kwa takribani zaidi ya miaka 17 na kulazimishwa sare ya bao 1-1 katika dakika 90 za mchezo.

Bao bora katika mchezo huo likifungwa na kijana wa wanapaluhengo, Seif Abdallah Karihe aliyenyumbulika mithili ya zama za Cristiano Ronaldo wa Manchester United kisha kutoa pasi kabla ya kurudishiwa mpira huo na kufunga bao safi na kuiongozea Lipuli FC lakini muda mchache mchezaji wa Young Africans, Donald Dombo Ngoma akaisawazishia timu yake kwa kuunganisha kwa kichwa kona iliyopigwa na Juma Abdul.

Kufuatia matokeo hayo mchezaji wa Yanga SC Kiungo wa kimataifa wa Zimbabwe, Thabani Michael Kamusoko ameonyesha kukerwa na matokeo hayo waliyoyapata.

Kamusoko mwenye umri wa miaka 29, amesema hafurahishwi na matokeo yaliyopatikana katika mchezo wao dhidi ya Lipuli mchezaji huyo ameyasema hayo alipohojiwa na chombo cha habari cha Azam Sports mara baada ya kumalizika kwa mchezo wao.

“Sikufurahishwa na matokeo tuliyoyapata leo (jana) ila mchezo umemalizika tunamuachia mwalimu” amesema Kamusoko kupitia Azam Sports.

Lipuli FC ndiyo timu pekee iliyopata point moja kati ya timu tatu zilizopanda dara msimu huu na kushiriki ligi kuu Tanzania Bara.

Okwi atupia 4, Simba SC Vs  Ruvu Shooting

Matokeo ya sare 1-1 ya Yanga SC dhidi ya Lipuli FC katika mchezo wao wa ufunguzi wa ligi umezidi kuchochea utani wajadi baada ya mahasimu wao Simba SC kuchomoza na ushindi mnono wa mabao 7-0 mbele ya timu ya Ruvu Shooting huku mchezaji wa kimataifa wa Uganda, Emmanuel Arnold Okwi akitupia mabao manne peke yake.

By Hamza Fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents