Habari

Kangi Lugola apokea kwa mikono miwili uamuzi wa Rais Magufuli, sasa kuelekeza nguvu zake jimboni kwake (Video)

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amemshukuru Rais John Magufuli kwa kumwamini na kumteua kushika wadhifa huo na kuongeza kuwa amepokea kwa mikono miwili uamuzi wa Rais wa kukaa kando katika nafasi hiyo na sasa atapeleka nguvu zake katika kuwatumikia wananchi wake wa Jimbo la Mwibara.

Lugola amesema hayo baada ya Rais Magufuli kuzungumzia kusikitishwa kwake na utendaji wa Wizara hiyo ya Mambo ya Ndani iliyoingia mkataba tata unaokadiriwa kuwa wa shilingi zaidi ya Trilioni Moja chini ya uongozi wake kama waziri.

Rais Magufuli aliweka wazi sakata hilo wakati wa uzinduzi wa nyumba za Magereza zilizopo Ukonga Jijini Dar es Salaam.

Source: Azam TV

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents