Habari

Kanisa jipya laanzishwa nchini Kenya maalum kwaajili ya watu maarufu na wenye pesa!

Kanisa jipya limeanzishwa nchini Kenya kwa lengo la kutoa huduma ya neno la Mungu kwa aina fulani tu ya watu ambao ni watu maarufu ‘celebrities’ pamoja na watu wenye pesa. Kanisa hilo limepewa jina la The All-Star Church.

laico-nightLaico Regency

Kwa mujibu wa taarifa ya Cate Mukei katika mtandao The-Nairobian, kanisa hilo ambalo limezinduliwa Jumapili iliyopita (July 7) litakuwa likitumia ukumbi wa hotel yenye hadhi ya nyota 5 Laico Regency iliyoko Nairobi, na linawalenga wanamuziki, wanamichezo mastaa, waigizaji, wanasiasa wa ngazi za juu, na watu wa Corporate.

Pasta mkuu wa ‘The All-Star Church’ Catherine Munene, ameuambia mtandao wa The Nairobian kuwa, hawatafuti watu maarufu wala hawawawindi, isipokuwa wanawahimiza kwenda kuabudu katika kanisa hilo sababu wanatoa huduma inayoendana nao. “We are not looking for celebrities or hunting for them. But we are encouraging them to come as we are offering what is relevant.”

Pia pasta huyo mwanamke alikanusha uvumi kuwa wamepewa ukumbi huo wa hotel bure na kusisitiza wanaulipia pesa nyingi “We are paying a lot of money which of course I cannot disclose. Please don’t listen to rumours that could destroy my church. I know media houses destroy churches and if The Nairobian does this we will deal with you. We are very powerful,” Alisema pasta Munene.

Kazi kwenu mastaa wa Nairobi.

Picha: Standard Digital

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents