Burudani

Kanye amtungia mtoto wa Jay Z, Blue Ivy wimbo maalum wa kumlaza (lullaby) kama zawadi ya birthday

Kanye West ameandika wimbo wa kumlaza (lullaby) mtoto Jay Z na Beyoncé, Blue Ivy.

Kanye-West (1)

Rapper na producer huyo ameitoa zawadi hiyo kwa Blue aliyetimiza miaka miwili January 7 kwakuwa alitaka kumpatia kitu ‘binafsi’ mtoto huyo wa rafiki yake. Chanzo kimoja kimeliambia gazeti la Daily Star kuwa wimbo huo hautatoka na ni kwaajili ya Blue tu. “Ana matumaini kuwa wimbo huo umtafanya Blue alale usiku,” kilisema chanzo hicho.

Chanzo hicho kiliongeza kuwa kwenye wimbo huo Kanye anarap jinsi Blue Ivy na mwanae North aka Nori watakuwa watu wakubwa na muhimu wakiwa wakubwa. “Unaongelea pia jinsi yeye na Jay Z watajituma kuhakikisha kuwa mabinti hao wanakuwa na maisha mazuri kuliko yalivyokuwa kwao.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents