Burudani

Kanye West: Wamarekani weusi walipenda kuwa watumwa

Msanii wa muziki wa Hip Hop kutoka nchini Marekani Kanye West amesema kuwa utumwa wa Wamarekani weusi uliofanyika zaidi ya miaka 100 iliopita lilikuwa chaguo lao.

Watu weusi walilazimishwa kutoka Afrika na kuelekea Marekani katika karne za 17, 18 na 19 na kuuzwa kama watumwa.

Kanye alinukuliwa na mtandao wa TMZ kwamba, haiwezekani watu wakubali kutawaliwa kwa miaka zaidi ya 400 bila kufanya chochote.

“Unaposikia kwamba utumwa ulifanyika kwa zaidi ya miaka 400.. miaka 400? ni kama walipendelea hilo kufanyika’, alisema katika tovuti ya burudani ya TMZ.

West baadaye alituma ujumbe wa Twitter na kusema kwamba hakueleweka vyema na kwamba alizungumza kuhusu miaka 400 kwa sababu ‘fikra zetu’ haziwezi kufungwa kwa miaka mingine 400.

Katika mahojiano na TMZ West alisema hivi sasa tunachagua kufanywa watumwa swala lililozua hisia kali kutoka kwa mfanyakazi mmoja mweusi katika kampuni hiyo.

Bwana Lathan alisema kuwa matamshi ya msanii huyo yalionekana kutolewa bila kufikiria.

“Una haki ya kuamini chochote unachotaka , lakini ujue kuna ukweli katika dunia ya sasa na athari zake kwa kila kitu ulichosema’, aliongezea huku nyota huyo akisimama na kujikuna kidevu.

“Lazima tukabiliane na ukandamizaji uliotokana na mika 400 ya utumwa ambayo ulisema kuwa watu wetu walipendelea, bwana Lathan aliendelea akiongezea kwamba nimeshangazwa na ndugu yangu nimeumizwa kwa wewe kusema kitu ambacho sio cha kweli.

Katika mahojiano hayo ya TMZ West amemtaja bwana Trump kuwa rafiki yake na kusema kuwa rais huyo ni miongoni mwa watu wake anaowapenda sana.

Matamshi yake yalizua hisia kali katika mitandao ya kijamii huku watumiaji wa mtandao wa twitter wakisema kuwa msanii huyo anafaa kusoma upya vitabu vya historia.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents