Burudani

Kanye West amporomoshea maneno ya hatari Drake ‘mimi na familia yangu tukiuawa, wewe umehusika’

Rapa Kanye West kutoka Marekani amemshambulia Drake kwenye mtandao wa Twitter kwa kile alichodai kuwa amepigiwa simu za vitisho kutoka kwa mkali huyo wa God’s Plan.

Kanye West alianza kwa ku-tweet kuwa amepokea simu za vitisho kutoka kwa Drake, kisha akaendelea kuandika kuwa kwa sasa endapo yeye na familia yake watapata matatizo basi Drake ndiye atakayekuwa muhusika.

https://twitter.com/kanyewest/status/1073409789827387392
https://twitter.com/kanyewest/status/1073410452250681344

Kanye West aliendelea ku-tweet kwa kuzungumzia uhasama uliopo kwa wasanii weusi nchini Marekani, kuwa ndio chanzo cha wao kuishia jela au kuuawa na kuendelea kutawaliwa na watu weupe. Akitolea mfano kwa marehemu XXXTentacion na Tekashi 69 ambaye yupo jela kwa sasa.

https://twitter.com/kanyewest/status/1073410829867982848

https://twitter.com/kanyewest/status/1073411988099907585

Kwenye muendelezo huo wa tweet zake, Kanye West amesema anamuomba Drake aachane na familia yake kwani kwa upande wake huu sio mwaka mzuri kwake atamchanganya kiakili.

https://twitter.com/kanyewest/status/1073418628014448640

https://twitter.com/kanyewest/status/1073419195528998912

https://twitter.com/kanyewest/status/1073419343176892416

Sababu kubwa ya Kanye West kumporomoshea Drake maneno hayo mazito, imeelezwa kuwa Drake aliandika mashairi ya kumdisi kwenye wimbo wa SICKO MODE wa Travis Scott.

Hata hivyo, vyombo vya habari nchini Uingereza vimeeleza kuwa maneno hayo yamechagizwa na tetesi za Kim Kardashian kutembea na Drake.

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents