Burudani

Kanye West anaamini kujiingiza kwake kwenye Siasa hakuwezi kuathiri biashara yake ya uuzaji wa viatu

Kanye West anaamini kujiingiza kwake kwenye Siasa hakuwezi kuathiri biashara yake ya uuzaji wa viatu

Rapper wa muziki kutoka Marekani Kanye West amefunguka kutokana na kile kinachosemekana kujiingiza kwake kwenye siasa kumeathiri sana biashara yake ya viatu.

Kanye licha ya kukiri kuwa alijihusisha na masuala ya kisiasa lakini pia alitangaza kuacha kabisha kujihusisha tena na siasa, ni baada ya kusema kuwa “alikuwa anatumika na Rais Trump kueneza ujumbe wenye chuki na ukakasi jambo ambalo haikuwa idhini yake”.

Licha ya kuwa mstari wa mbele kuukingia kifua uongozi wa Rais Trump, amesema kuwa kwa sasa atajikita kwenye mambo yake binafsi ya ubunifu na atajiweka mbali na siasa.

Lakini pia amefunguka kuhusiana na kushuka kwa mauzo katika biashara yake ya viatu,hii ni baada ya kutolewa kwa toleo jipya aina ya YEEZY BOOST 700 “Mauve” ambalo halijafanikiwa kufanya vizuri sokoni ikilinganishwa na matoleo ya zamani ya viatu hivyo (sneaker). Wengi wamesema kwamba sababu ya mauzo dhaifu ni kutokana na Ushirikiano wake na Rais wa nchi hiyo Donald Trump na kuonekana kuanza kutoa maoni yake juu ya siasa. Vyanzo vya karibu na Kanye na timu yake wamekataa uvumi huu, na wameendelea kusema kuwa mauzo yalikuwa sawa lakini viatu ni vingi zaidi vilivyotengenezwa ikilinganishwa na aina zilizopita.

kinachotakiwa ni kwamba tutatakiwa kusubiri  YEEZY 500 ambayo inatarajiwa kutolewa mnamo Novemba 30 ili kujua kama hii itakuwa kama hali inayoendelea ingawa vyombo vya habari vya karibu zaidi kwa Kanye, vikidai yeye amewekwa kwenye collab na Big Baller Brand.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents