Burudani

Kanye West atoa msaada kwa watoto yatima Uganda, amjibu Bebe Cool kuhusu kolabo (+video)

Rapper Kanye West kutoka Marekani jana Jumanne alitembelea kwenye kituo kikubwa cha watoto yatima mjini Wakiso nchini Uganda kiitwacho Masulita Children’s Home.

https://twitter.com/kanyewest/status/1052137531880497152

Kanye akiwa kwenye kituo hicho, alitoa msaada wa pea za viatu vya Yeezy, Fedha na spika ndogo za Bluetooth kwa ajili ya kusaidia watoto hao kusikilizia muziki.

Kanye West na familia yake walipelekwa na Helikopta binafsi kutoka Kampala hadi Wilayani Wakiso huku wakilindwa na Wanajeshi kwa ajili ya usalama zaidi.

Akiongea na waandishi wa habari baada ya tukio hilo, Kanye West aliuliza swali kuhusu maombi ya kolabo ya msaani wa Uganda, Bebe Cool “Umefika Uganda Je, kuna chochote umefanya na Bebe Cool kuhusu maombi yake ya kufanya kolabo?” lilihoji swali na kisha Kanye akajibu kwa mkato “Ndio, ndio tutafanya” .

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents