Burudani

Kanye West na Rick Rubin kutayarisha album ya Justin Bieber

Justin Bieber yupo mbioni kumaliza kurekodi album yake mpya kwa msaada wa watayarishaji nguli, Kanye West na Rick Rubin.

Justin-Bieber-Red-Michael-Jackson-Thriller-Leather-Jacket-Kanye-West-Adidas-Show-800x962

“Sitaki kusema kuwa ni tofauti sababu hicho ndio kila mtu anasema. Lakini ni tofauti, ni version ya kikubwa ya Justin na nadhani watu watashtuka,” staa huyo ameliambia USA Today.

Bieber amedai kuwa mabadiliko katika namna anavyoishi kufuatia kuhusika kwenye vitendo vingi vya utovu wa nidhamu siku za nyuma, yatasikika kwenye muziki wake.

“Muelekeo wangu wote umebadilika. Kile unachofikiria muda wote ndicho unachoandika na sasa kwakuwa nafikiria mambo chanya zaidi, kimebadilisha muziki wangu.”

Bieber amesema album yake ilikuwa imekamilika lakini aliamua kuirekodi upya kwendana na maisha yake ya sasa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents