Kapuya kusuluhisha mgogoro Reli leo

WAZIRI wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Profesa Juma Kapuya, leo anatarajia kukutana na uongozi wa wafanyakazi wa Shirika la Reli Tanzania

Halima Mlacha


 


WAZIRI wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Profesa Juma Kapuya, leo anatarajia kukutana na uongozi wa wafanyakazi wa Shirika la Reli Tanzania (TRL) kujadili nao namna ya kumaliza mgogoro wao na menejimenti ya shirika hilo.


Akizungumza na gazeti hili jana, Profesa Kapuya alisema tayari ameshakutana na menejimenti ya shirika hilo jana na kwa kuwa suala hilo ni shirikishi hawezi kueleza chochote hadi atakapokutana na pande zote.


Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu, Omary Chambo, ambaye alishuhudia utiaji saini wa makubaliano ya pande zote mbili ya juu ya kuanza kulipwa rasmi mshahara wa kima cha chini wa Sh 160,000 mwezi uliopita, alisema tatizo hilo litamalizika kwani mazungumzo yanaendelea.


“Kwa sasa pande zote zinaendelea na mazungumzo na Bodi ya TRL inatarajia kukutana kwa ajili ya ku-solve suala hili, sisi ni wawezeshaji tu,” alisema Chambo. Hata hivyo, kwa mujibu wa tangazo lililotolewa jana na menejimenti ya shirika hilo, safari za Bara za treni zimesitishwa kutokana na tishio la mgomo wa wafanyakazi wa TRL baada ya saa 48.


Juzi wafanyakazi wa TRL kupitia chama chao cha TRAWU, walitoa notisi ya siku 48 inayomalizika kesho kwa uongozi wa shirika hilo, kuchukua hatua mara moja za kulipa kiwango cha mshahara mpya walichokubaliana kuanza kulipwa Machi, mwaka huu, vinginevyo watagoma nchi nzima.


 


Source: Habari Leo

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents