Habari

Kardinali matatani kwa unyanyasaji wa kingono

By  | 

Polisi nchini Australia imemshtaki Kardinali wa kanisa katoliki George Pell, kwa makosa kadhaa ya kuwanyanyasa watoto kingono.

KardinaliPell ambaye ni mweka hazina wa Vatican na kiongozi mkuu wa kanisa katoliki nchini Australia, anatarajiwa kufika mahakama ya Melbourne mwezi Julai ili kujibu mashtaka hayo yanayomkabili.

Polisi waliamua kuchukua hatua za kumshtaki Kardinali Pell, baada ya kupata ushauri kutoka kwa viongozi wa mashtaka mwezi uliyopita. Kardinali huyo sio mkuu wa kanisa katoliki nchini Australia bali pia ni miongoni mwa viongozi wakuu walio na hadhi ya juu katika ulimwengu wa kanisa hilo.

Kardinali Pell mwenye makao makuu yake Vatican,amekana madai hayo ambayo yanasemekana kufanyika miaka ya 1970. Na atarudi nchini Australia haraka ili kujisafishia jina lake na madai hayo pia ameyakana licha ya kukubali kufika mahakamani mwezi ujao.

Na Laila Sued

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments