Habari

Kardinali Pengo achukizwa na matanuzi

Askofu Mkuu wa Jimbo la Katholiki Jimbo kuu la Dar es salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amewataka waumini wa madhehebu hayo kutotumia muda na mali zao kufanya sherehe kubwa badala yake watumie muda huo kujenga makanisa.

2
Askofu Mkuu wa Jimbo la Katholiki Jimbo kuu la Dar es salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.

Alitoa kauli hiyo hivi karibuni alipokuwa mgeni rasmi kwenye harambee ya kuchangia shilingi milioni 50 kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa Katoliki Tumbi, Kibaha mkoani hapa. Kardinali Pengo alisema ili wanadamu waishi kwa furaha, upendo na amani wanapaswa kupewa ujumbe wa neno la Mungu wakiwa kwenye mazingira bora, hivyo ni vyema jitihada za dhati zikafanyika kujenga makanisa zaidi.

“Nakushukuru Padri Beno (Kikudo) wa kanisa hili ambaye uliona ni vyema utumie siku ya maadhimisho ya miaka yako 50 ya kuzaliwa kufanya harambee hii kukusanya fedha za kukamilisha ujenzi wa kanisa, kuliko wengine ambao wamekuwa wakitumia sherehe hizo maeneo ya fukwe za bahari,” alisema. Alisema makusudi ya Mungu siyo kufuja mali ambazo anawajalia wanadamu, bali kutumia mapato yao kwenye mambo ya maendeleo.

Padri Kikudo aliwashukuru waumini kwa kuonyesha juhudi na moyo wa michango ya hali na mali tangu ujenzi wa kanisa hilo ulipoanza.

BY: EMMY MWAIPOPO

CHANZO: MWANANCHI

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents