Kasi za Dogo Janja

Abudalazizi Chende aka Dogo Janja msanii mdogo sana mwenye kipaji kikubwa cha kuimba, anayekuja kwa kasi ya ajabu katika fani ya muziki chini ya wakali wa Tip Top connection.

Dogo Janja leo aliongea na Bongo5 jijini Dar es Salama na kusema kuwa tayari ameshatoa singo moja ya ‘Anajua’ aliyemshirikisha Tunda na Madee  ambayo kwa sasa inapigwa katika vituo vya redio hapa nchini, ambayo msanii huyo yuko mbioni kuifanyia video tayari kwa kuirusha hewani.Dogo anatarajia kutoa wimbo mwingine mpya ‘Tulia’ hivi karibuni akiwa amemshirikisha mkali wa rhymes, Joh Makini.

Dogo mwenye umri wa miaka 13 na tatu  na alianza kuimba akiwa darasa la tatu baada ya mwalimu wa somo la Stadi za kazi kuwaambia kila mtu abuni kitu ambacho atafanya akatunga wimbo  wa UKIMWI ambao uliweza kumshangaza mwalimu na wanafunzi wenzake hvyo wote kutambua kipaji cha dogo.

Msanii huyo alishiriki katika mashindano ya TAU yaliofanyika mwaka 2007 mjini Arusha akiwa darasa la tano  na alibahatika kuwa  mshindi wa kwanza na akiwa ndiye mwenye umri mdogo katika mashindano hayo, na kupata zawadi ya kurekodi nyimbo moja ya  ‘Sijafikia’ ingawa haikuweza kutemba sana.

Dogo Janja anatarajia kuanza elimu yake ya sekondari mapema 2011 na amesema kuwa anatarajia kujikita na masomo zaidi kwani muziki ni kipaji ailichonacho na hakiondoki.

Bongo5 inampa shavu dogo, Big Up Yourself!

Sikiliza wimbo wa Anajua ya Dogo Janja akiwashirikisha Tunda Man na Madee hapa chini:

{mmp3}mangi_mic_ft_tunda_man_anajua.mp3{/mmp3}

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW