Burudani

Kassim Mganga aeleza jinsi alivyochukua siku nyingi kurekodi wimbo wake mpya ‘Somo’ na live bendi

Mkali wa nyimbo za mahaba Kassim Mganga amesema wimbo wake mpya ‘Somo’ ambao ameuachia hivi karibuni akiwa amemshirikisha Nyota pamoja Kilimanjaro Band (Njenje) ni wimbo wake wa kwanza ambao ameurekodi na live bendi.

Muimbaji huyo amedai wimbo huyo umeuandaa kwa kipindi cha miaka miwili mpaka unatoka huku akidai mazoezi ya bendi pekee alifanya kwa mwezi mmoja.

“Unajua huu wimbo ulikuwa utoke hata kabla ya Subira, lakini mambo yakawa mengi hasa hasa katika harakati za kuuandaa, Kilimanjaro Band walikuwa busy muda mwingi sana,” Kassim alikiambia kipindi cha FNL cha EATV. “Mazoezi tu hata kabla ya kuanza kurekodi tumefanya mwenzi mmoja, kwa hiyo kusema kweli mpaka kazi inakamilika na kutoka haikuwa kazi rahisi,”

Wimbo huo ambao video yake imeachiwa jana, umepokelewa kwa shangwe kubwa na mashabiki huku baadhi ya wasanii kama Fid Q wakionyesha kuukubali wimbo huo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents