Burudani

Kat DeLuna afunika Leaders

Mwana Dada toka nchini Marekani Kat DeLuna, usiku wa kuamkia jumapili aliweza kuwapagawisha maelfu ya Mashabiki waliojitokeza katika Tamasha la Fiesta 2008 “Kujiramba”, lililofanyika katika viwanja vya Leaders Club

Kat DeLuna afunika Leaders

 

Mwana Dada toka nchini Marekani Kat DeLuna, usiku wa kuamkia jumapili aliweza kuwapagawisha maelfu ya Mashabiki waliojitokeza katika Tamasha la Fiesta 2008 “Kujiramba”, lililofanyika katika viwanja vya Leaders Club.

 

Ilikuwa majira ya saa 7.45 usiku ambapo mwana dada huyo mahiri kwa kupiga shoo za nguvu huku akicheza kwa umahiri na kuimba kwa sauti tamu ya kuvutia alipotinga jukwaani na kuanza kuwasalimia Maelfu ya Washabiki waliojitokeza viwanjani hapo tayari kwa Kujiramba.

 

Mwanadada huyo anayetamba kwa sasa na kibao chake cha “Run the show”, aliweza kuamsha kelele na shangwe kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam na vitongoji vyake pale alipopanda jukwaani tayari kwa kuanza shoo ambapo kitu cha kwanza alichokifanya ni kuwaamuru watanzania kupiga kelele zaidi juu ya ushindi wa Rais mpya wa Marekani Barack Obama.

 

Mwanadada huyo alipaza sauti na kusema “Hallo Tanzanians Clap for Obamaaaaa” alipiga kelele hizo kwa kushangilia mbele ya watanzania, kitu ambacho washabiki nao wakawa ndiyo kama kitu walichokuwa wakikisubiria kukisikia kwa Kat Deluna ambapo nao bila kusita walipiga mayowe yaliyotikisa hali ya jiji huku baadhi yao wakipiga makelele kwa staili mpya za aina yake huku wengine wakitokwa na machozi.

 

Kat DeLuna afunika Leaders

 

 

Tamasha hilo la Fiesta 2008 lililoandaliwa na kampuni kubwa ya Prime Time Promotions pamoja na udhamini mkubwa wa mtandao wa simu za mkononi hapa nchini Zain, sambamba na Bia ya Kilimanjaro premium Lager liliweza kuvutia zaidi kutokana na shoo kali za madensa wake mapacha wa kiume kulishambulia jukwaa kwa pamoja hali iliyopelekea kelele za mashabiki kuongezeka huku wakisukumana na mabaunsa ili waweze kulisogelea jukwaa na kumgusa Dada huyo ambapo walishindwa kutokana na nguvu na maharifa kutoka kwa mabaunsa hao.

 

Hali ilizidi kuwa pevu zaidi kwa mabaunsa pale ambapo mwana Dada huyo alipoanza kutumbuiza kibao chake kinachotesa kwa sasa kiitwacho “Run the Show” alichomshirikisha gwiji wa miondoko ya Rap nchini Marekani Busta Rhymes, ambapo washabiki walionesha kupagawa zaidi na kutafuta namna ambayo wangeweza kuwapenya mabaunsa hao na kufika jukwaani hata kumgusa nyota huyo wa kike kutoka nchini Marekani.

 

Hadi anashuka jukwaani yapata majira ya saa 8.52, mwana Dada huyo aliweza kukata kiu kubwa ya Maelfu Mashabiki hao waliohudhuria Tamasha hilo huku kila mmoja akionyesha furaha ya KUJIRAMBA kwa nguvu.

 

Tamasha hilo kubwa la Fiesta 2008 lilisindikizwa pia na wanamuziki kibao wanaotesa nchini kama Jay Mo, Joh Makini, Mwana FA, Ngwair, Professor Jay, Dully Sykes, Mr.Blue, Dogo Mfaume, Matonya, Mwasiti, Maunda Zoro na wengine kibao ambao walilifanya Tamasha hilo kuwa tamu zaidi kutokana na “Full Majirambo” yaliandaliwa na wadhamini wa Fiesta mwaka 2008.

 

Video na picha zaidi zitaanikwa karibuni.

 

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents