Tia Kitu. Pata Vituuz!

KATAVI: Mkandarasi akamatwa kwa kuvunja madirisha ya kituo cha afya akidai kutokulipwa

KATAVI: Mkandarasi akamatwa kwa kuvunja madirisha ya kituo cha afya akidai kutokulipwa

Mkandarasi aliyefahamika kwa Borniface Exavery, ambaye alitengeneza madirisha ya Almunium na katika Kituo cha Afya cha Katumba, Halmashauri ya Nsimbo ya mkoani Katavi, ameyavunja madirisha hayo, kwa kile alichokidai kutokamilishiwa malipo yake na ofisi ya Halmashauri huku akiwa ameshamaliza kazi.

Akizungumza mara baada ya kutembelea eneo hilo, Mkuu wa Mkoa wa Katavi Juma Homera, amedai mradi huo ulikuwa umekiuka taratibu mbalimbali za kisheria, ikiwemo upatikanaji wa tenda hiyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, mwenyewe ameeleza kushtushwa na hatua ya Mkandarasi huyo, na kueleza taarifa za awali walizipata kutoka kwa wananchi, na kulitaka Jeshi la Polisi kumshikiria Mkandarasi huyo, huku akikiri Halmashauri kutomlipa malipo yake.

Mmoja wa Wakandarasi ambaye anajulikana kama Bulaya Mushi, ambaye na yeye anaidai Halmashauri hiyo kwenye mradi huo wa Kituo cha Afya, amemuomba Mkuu wa Mkoa kuangalia madai yao ili waweze kulipwa na Halmashauri hiyo.

Chanzo Eatv.tv

 

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW