Burudani ya Michezo Live

KATAVI: Mume na Mke wauawa kikatili kwa kukatwa mapanga baada ya kuvamiwa usiku, Dada asimulia ilivyokuwa – Video

KATAVI: Mume na Mke wauawa kikatili kwa kukatwa mapanga baada ya kuvamiwa usiku, Dada asimulia ilivyokuwa - Video

Noel Mswanya na Stela kisanga ambao ni Mume na Mke wakazi wa Mtaa wa Nsemulwa wilayani Mpanda mkoani Katavi, wameuawa kwa kukatwa mapanga, baada ya kuvamiwa na watu wanaodhaniwa ni majambazi usiku wa kuamkia leo.

Askari wakifanya shughuli ya kuokoa miili ya marehemu

Tukio linatajwa kutokea saa saba usiku wa kuamkia Disemba 16, 2019 katika Kata Nsemulwa mkoani Katavi, ambapo inasemekana majambazi hao walivamia nyumba hiyo na kuwauwa wapenzi hao.

Akizungumzia tukio hilo Dada wa Marehemu Noel Mswanya, Joyce Mswanya “nimepigiwa simu saa 12 : 30 usiku na Mjumbe wa Serikali ya Mtaa, kuwa mdogo wangu Noel ameshauawa, na nilimkuta wifi yangu na yeye ameuawa akiwa nje ya nyumba

Naomba sana Serikali isaidie kuwatafuta wahusika wa tukio hili ili ikiwezekana wakamatwe wachukuliwe hatua za kisheria” ameongeza Joyce mswanya

Kwa mujibu wa Eatv.Tv Juhudi za kumtafuta Kamanda wa Polisi Katavi bado zinaendelea.

View this post on Instagram

KATAVI: Mume na Mke wauawa kikatili kwa kukatwa mapanga baada ya kuvamiwa usiku, Dada asimulia ilivyokuwa : Noel Mswanya na Stela kisanga ambao ni Mume na Mke wakazi wa Mtaa wa Nsemulwa wilayani Mpanda mkoani Katavi, wameuawa kwa kukatwa mapanga, baada ya kuvamiwa na watu wanaodhaniwa ni majambazi usiku wa kuamkia leo. Askari wakifanya shughuli ya kuokoa miili ya marehemu Tukio linatajwa kutokea saa saba usiku wa kuamkia Disemba 16, 2019 katika Kata Nsemulwa mkoani Katavi, ambapo inasemekana majambazi hao walivamia nyumba hiyo na kuwauwa wapenzi hao. Akizungumzia tukio hilo Dada wa Marehemu Noel Mswanya, Joyce Mswanya “nimepigiwa simu saa 12 : 30 usiku na Mjumbe wa Serikali ya Mtaa, kuwa mdogo wangu Noel ameshauawa, na nilimkuta wifi yangu na yeye ameuawa akiwa nje ya nyumba” “Naomba sana Serikali isaidie kuwatafuta wahusika wa tukio hili ili ikiwezekana wakamatwe wachukuliwe hatua za kisheria” ameongeza Joyce mswanya Kwa mujibu wa Eatv.Tv Juhudi za kumtafuta Kamanda wa Polisi Katavi bado zinaendelea. : Video credit by Eatv.tv. WRITTEN BY @el_mandle

A post shared by bongo5.com (@bongofive) on

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW