Burudani

Kati ya Kendrick Lamar na Dr Dre, Dogo Janja anamkubali huyu…

Msanii kutoka Tip Top Connection, Dogo Janja amefunguka na kusema kati ya Kendrick Lamar na Dr Dre, yeye anamkubali zaidi Dr Dre kwa sababu muziki wao unaeleweka kirahisi na hauna matabaka.

Dogo Janja

Dogo Janja alikiambia kipindi cha Clouds Fm Top 20 kuwa muziki wa Dr Dre kila mtu anaweza kuusikiliza ukilinganisha na ule wa Kendrick Lamar ambao unachagua baadhi ya watu.

Kendrick Lamar na Dr Dre

“Albamu ya Kendrick ninayo, ni kali lakini kuna saa nikilisikiliza nakutana tu na mawe magumu, kuna dude lake moja ndio kaimba ndio tu nalikubali. Kuna nyimbo zake hata majina hayakaririki. Yeye ana fan base yake lakini mimi kwa hapo kura ya yangu natoa kwa Dre,” alisema Dogo Janja.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents