Habari

Katiba tarajiwa ni aibu tarajiwa au tumaini tarajiwa?

By Mark Rose Msemwa

Nimeguswa kuandika makala hii kutokana na kinachoendelea na ninachokiona kuwa watu wote walio katika Bunge maalum la Katiba wana nia ya dhati kabisa na inayolitakia mema Taifa letu. Ila naamini kuwa kuna swali huenda tunasahau kujiuliza nalo ndilo lililoandikwa kwa herufi kubwa hapo juu. Kwangu mimi, itakuwa ni aibu kubwa kama tutakuja na katiba ambayo uzao wetu wa kwanza tu, utaanza kuitia viraka katiba hii, jambo ambalo hatulioni kwa nchi zilizoendelea.

Samuel_Sitta

Japo litakuwa ni jambo la faraja sana na litakalo wafanya wajumbe wote na kizazi cha leo kutembea kifua mbele kwa kwa ubora wa Katiba iliyopo na ambayo tumeshiriki kuijadili na kuipitisha. Suala hili litafanikiwa iwapo tu, Wabunge wa bunge maalumu la katiba watazingatia yafuatayo, japo neno langu si la kitabu kitakatifu;

1; Wajumbe kutambua kuwa, Katiba hii tutakufa tutaiacha. Na hivo si kwaajili yetu tuliopo tu.
2; Japo wajumbe mnawakilisha taasisi mbali mbali ila Katiba hii sio mali ya taasisi unayoiwakilisha.
3; Mjumbe huna mkataba wa milele na taasisi iliyokupendekeza, wewe ni mtu huru uishie kwenye nchi huru na maisha yako, taaluma yako na mapenzi yako yanaweza kubadilika muda wowote, kama unatetea wakulima na ukasahau kuna wafanyabiashara, huenda ukitoka humo ndani ukawa na mtazamo wa kibiashara na ukaenda kukutana na yale ulio yasahau. Kama uko CUF usisahau kuwa muda wowote unaweza kuwa TLP kwani tushayaona hayo.

4; Usije ukamkandamiza mwanamke kwenye katiba ukasahau kuwa una mtoto wa kike au bado unazaa, au ukamkandamiza mwanaume ukasahau kuwa mumeo kipenzi ni mwanaume, una mtoto wa kiume au bado unazaa.

MCHANGO WANGU

1; Kuwa na Mfumo wa vyama vingi haimaanishi tusiwe na kikomo cha idadi ya vyama. Kuwa na msululu wa vyama ni kuwa na msululu wa tofauti za mawazo yetu na yanayopelekea tofauti zetu.

2; Kutilia mkazo malezi bora kwa watoto miaka 0-7.

Mungu ibariki Tanzania na watu wake. Kila la heri Wajumbe wetu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents