Habari

Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda Dkt. Adelhelm Meru afurahia ujio wa Jotun

Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Adelhelm Meru amezindua duka la vifaa vya Ujenzi la Jotun Tanzania, lililopo Mtaa wa Mkwepu, Posta Mpya jijini Dar es salaam.

Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dr. Adelhelm Meru (watatu kutoka kulia ) akikata utepe katika ufunguzi wa Jotun Tanzania akiambatana na Balozi wa Norway Bibi Hanne Marie Kaarstad (wapili kutoka kulia)

Akizungumza katika uzinduzi huo, Dkt Meru amesema uwekezaji huo utakuwa ni chachu katika Tanzania ya Viwanda.

“Sisi kama serikali tunawakaribisha sana nchini Tanzania, tena mmekuta tuna sera ambazo ni rafiki kwa uwekezaji zaidi. Na habari njema ni kwamba tayari nimezungumza nao na wao wamesema wanaangalia biashara kwa miaka hii michache na baadaye wakishapata wasoko watafungua kiwanda kabisa hapa nchini,” alisema Dkt. Adelhelm.

Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dr. Adelhelm Meru, akipewa maelekezo ya namna mashine ya uchanganyaji rangi inavyofanya kazi toufauti kwa dakika moja.

Kampuni ya Jotun iliyoanzishwa nchini Norway mwaka 1926, ni moja ya kampuni zinazoongoza katika uzalishaji wa rangi duniani, ambapo mwaka 1974 Jotun waliweka uwepo wao katika nchi za umoja wa nchi za kiarabu, tangu wakati huo Jotun imekuwa ikikuwa katika maeneo tofauti, na kuwa kampuni pekee ya uzalishaji rangi  iliyopata tunzo ya vyeti vya viwango vya ubora vyenye  namba  ISO 9001: 2008, ISO 14001 & OHSAS 18001.

Kampuni hii pia ina viwanda vya uzalishaji katika nchi ya Abu Dhabi, Dubai, Saudi Arabia, Oman na Misri.

Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dr. Adelhelm Meru, akihutubia katika sherehe za ufunguzi wa duka la rangi ya Jotun Tanzania.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents