Aisee DSTV!
SwahiliFix

Katika kukabiliani na upinzani kwenye uchaguzi mkuu ujao, Mbunge aweka tangazo la kuomba kura kwenye website ya ‘Ngono’

Katika chaguzi nyingi huwa tunaona watu wanaogombea nafasi kubwa kwenye uongozi wanavyohangaika na Kampeni ili kujihakikishia ushindi, sasa hiyo huenda ikawa haitoshi kwa Mbunge mmoja nchini Denmark aitwaye Joachim B. Olsen ambaye ameamua kuweka bango la kuomba kura kwenye mtandao wa ngono.

Bw. Olsen  ameamua kuweka tangazo hilo la kampeni kwenye website hiyo ya ngono ijulikanayo kwa jina la PornHub, ili kukabiliana na wapinzani wake kwenye kinyang’anyiro cha uchaguzi mkuu ujao mwezi Juni mwaka huu.

Baada ya kuulizwa na Waandishi wa Habari, Olsen (41) amekiri wazi kuwa yeye ndiye aliyeweka tangazo hilo na kitendo hicho kimeungwa mkono na baadhi ya wabunge wa chama chake cha Liberal Alliance, ambao wamedai kuwa aina hiyo ya utafutaji wa kura, itamsaidia kupigiwa kura kwa wingi katika uchaguzi mkuu ujao.

Ni kweli tangazo limewekwa na mimi, Lengo kubwa ni kuwafuata wapiga kura wangu popote walipo. Najua na natambua kuna watu wamefurahia wengine wamechukizwa ila sikuwa na kusudio ovu bali ni katika kutafuta kura za uchaguzi ujao,” ameeleza Olsen.

 

 

 

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW