Burudani

Katy Perry ajitengenezea rekodi ya dunia kwenye Twitter

By  | 

Katy Perry ametengeneza rekodi mpya kwenye mtandao wa Twitter. Muimbaji huyo wa Marekani amekuwa mtu wa kwanza kufikisha followers milioni 100 kwenye mtandao huo.

Baada ya kufanikiwa kufikisha idadi hiyo, Twitter wamempongeza mrembo huyo kwa kumuwekea kipande cha video na kuandika, “Today, we #WITNESS history. Congratulations @katyperry, the first to reach 100 million followers! #LoveKaty.”

Hata hivyo Selena Gomez ambaye anaongoza kwenye mtandao wa Instagram kwa kuwa na followers milioni 122, ameachwa mbali kwa kuwa na followers milioni 48.3.

Kwa upande wa viongozi, aliyekuwa Rais wa Marekani Barack Obama ndio mwenye idadi ya watu wengi kwenye mtandao huo ambao ni follower milioni 90.9.

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments